Eti wadau nielewesheni hapa kwanini mara nyingi makosa akiyafanya @diamondplatnumz huyu binti(@officialzuchu) ndiye anaeshambuliwa sana...? au kosa lake kubwa ni kuwa na mahusiano na Diamond na pengine baadhi yenu hamjaridhika?
Bado nawaza @officialzuchu amewatengenezaje hawa maadui ambao wanashangilia na kumdhihaki mara kwa mara Diamond anapoonekana kuharibu mambo? ebu nipeni majibu.
Yote kwa yote @wcb_wasafi kama record label nadhani mna wajibu wa kuhakikisha huyu binti afya yake ya akili inakua sawa hizi dhihaka zinazoendelea mitandaoni dhidi yake sidhani kama anastahili wakati yeye ndiye victim,she's young,talented & blessed na tunamtegemea katika kuikuza industry ya muziki wa Afrika mashariki.