“Tunaposema bila mabadiliko hakuna uchaguzi tuna maana kwamba kusipokuwa na mabadiliko yanayohitajika ya mfumo wa uchaguzi tutafanya kila tunaloweza kwa nguvu tulizonazo kuhakikisha uchaguzi mkuu haufanyiki mwaka huu, hatuzungunzii kususia uchaguzi hatutosusia, tutaenda kuwaambia Watanzania na tutaiambia Jumuiya ya Kimataifa, tutawaambia Walimwengu kwamba kama CCM na Serikali yake haipo tayari kufanya mabadiliko ili kuwe na uchaguzi huru na haki, uchaguzi mwaka huu usifanyike kabisa ndio maana ya no reform no election”
“Huu sio uamuzi wa Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu, ni msimamo wa Chama cha CHADEMA”
“Natoa wito kwa Viongozi wetu wa Dini, Maaskofu, Mapadri na Masheikh wetu, na wao ni Watanzania, yakiharibika yanaharibika na kwao yakitengamaa yanatengamaa na kwao, wasikubali kuambiwa wajibu wao ni kuombea roho za Waumini wao tu, wajiulize je miili ya Waumini wao ipoje, wahangaike na njaa ya haki ya Waumini wao, wasikubali kuambiwa wasijihusishe na siasa kwasababu siasa ndio maisha yenyewe”
—— Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, akitoa hotuba kwa Taifa leo February 12,2025