Ukistaajabu ya Gamondi utaona ya Ramovic




Ukistaajabu ya Gamondi utaona ya Ramovic ni kauli ambayo unaweza kuitamka kufuatia ripoti zinazovuma kuhusu kuondoka kwa Sead Ramovic kama kocha mkuu wa Yanga Sc huku ikielezwa kwamba amepata dili Nchini Algeria.

Wakati Wananchi wakijiandaa kuivaa Ken Gold Fc kwenye mchezo wa Ligi Kuu bara kesho, leo jioni wakati wa mazoezi habari zimesikika kuwa Mjerumani huyo atafunga virago vyake na kuondoka klabuni kesho.

Ripoti zinaeleza kuwa Ramovic anaondoka klabuni hapo kwa makubaliano ya pande zote baada ya kupata ulaji kunako klabu ya CR Belouzidad ya Algeria akitarajiwa kuchukua mikoba ya kocha Abdelkader Amrani aliyeachana na timu hiyo Januari 25, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad