Lile dili la Sh 3 bilioni limeota mbawa. Ndicho unachoweza kusema baada ya miamba ya soka ya Libya 🇱🇾 Al Ettihad kuachana na mpango wa kumsajili straika wa Yanga, Clement Mzize 🇹🇿 na badala yake kunasa saini ya Tumisang Orebonye, raia wa Botswana.
Nyota huyo amejiunga na kikosi hicho akitokea AS FAR Rabat ya Morocco aliyo jiunga nayo Januari mwaka jana akitokea USM Alger ya Algeria akishinda taji la Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023 na USM Alger, sawa na CAF Super Cup 2023.
.
Kitendo cha nyota huyo kutua kwa miamba hiyo kimefanya dili la Mzize kukwama, licha ya kiasi kikubwa cha dola milioni 1.2 (Sh 3.1bilioni) ambacho Yanga ingekipata. Mzize amekuwa na kiwango bora akiwa na Yanga anayoitumikia kwa misimu mitatu sasa ambapo hadi sasa amefunga mabao tisa ya Ligi Kuu akiongoza mbio za ufungaji bora.