Klabu ya Al Masry maarufu kwa jina la Tai wa kijani ‘Green Eagle’ 🦅 ilianzishwa Machi 18, 1920 ikiwa ni moja kati ya timu tano bora kwa taifa la Misri ambapo Simba itatakiwa kujiandaa kupambana nayo kwa umakini kutokana na ubora wa kikosi chao.
.
Hata hivyo haina mafanikio nakubwa kwa michuano ya CAF na hata nyumbani ukilinganisha na vigogo ingine vya Misri. Mafanikio makubwa ya Al Masry katika mashindano ya klabu Afrika miaka ya hivi karibuni ni kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2018 baada ya kuitoa Simba raundi ya pili, ingawa pia imewahi kutinga hatua kama hiyo kwenye Kombe la Caf mwaka 2002.
.
Kwa msimu huu ilikuwa Kundi D ukimaliza nafasi ya pili ikifunga mabao saba na kuruhusu manne ikikusanya jumla ya pointi tisa kwenye kundi lililoongozwa na ndugu zao Zamalek Wakiwa na pointi 14. Kwenye mechi hizo sita za makundi, Al Masry ilishinda michezo miwili yote ya nyumbani dhidi ya Black Bulls ya Msumbiji (3-1) na Enyimba ya Nigeria (2-0), kisha ikatoa sare tatu na kupoteza mmoja dhidi ya Zamalek (1-0).
.
Kikosi hicho kinacho fundishwa na kocha mzawa Ali Maher (51) kinatumia mifumo mitatu tofauti 4-3-2- 1, 4-1-4-1 na 4-3-3 ikitegemea na ubora wa wapinzani wao wanaokutana nao kwenye mashindano.