Web

Wakala wa Fabrice Ngoma Afunguka Ngoma Kubakia Simba: Tunaangalia Mpunga tu




WAKALA wa Fabrice Ngoma, kiungo nyota wa Simba, Faustino Mukandila amesema maslahi mazuri zaidi ambayo kiungo huyo atawekewa mezani ndio yataamua kama ataondoka au kubaki Msimbazi.

Mukandila ametoa kauli hiyo baada ya Al Ittihad ya Libya kuonyesha nia ya kuhitaji huduma za nyota huyo wa zamani wa AS Vita Club ya DR Congo na Raja Casablanca ya Morocco.

Mukandila anayemsimamia pia Djibrill Sillah wa Azam FC alisema kuwa hadi sasa Ngoma hajasaini mkataba wowote iwe wa kubaki Simba au kuondoka na uamuzi wa hilo utategemea nguvu ya ushawishi.

“Hakuna chochote kilichofanyika kati yetu na Simba wala timu nyingine. Kwa sasa mchezaji yupo na Simba na ibakie kuwa hivyo, lakini kama ataondoka au atabaki ni suala muda sahihi ukifika uamuzi utafanyika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad