Wakala wa Mzize...Kumzuia Mzize ni Kumnyima Asiendelee



“Yanga imeweka kiasi cha pesa ambacho inataka kupata kwa kumuuza Mzize, kuweka kiasi na kukipata ni vitu viwili tofauti. Timu za England zina viwango vyao, wanaweza kusema hawawezi kutoa kiasi fulani cha fedha kwa sababu mchezaji anacheza Ligi Afrika na wakaweka kiwango ambacho wapo tayari kutoa.
.
Wydad waliweka dola za Marekani milioni moja (Sh 2.6 Bilioni) kiasi ambacho Yanga ilihitaji. Hiyo hata mimi waliniambia wapo tayari kutoa
.
Kumzuia Mzize kuondoka ni kumnyima kuendelea na kumnyima kupata maslahi zaidi ambayo hata wenyewe wanajua hataweza kuyafikia kutokana na mshahara ambao ameahidiwa huko nje.
.
Wydad Casablanca inamuhitaji sana Mzize na haijaanza sasa hivi bali ni muda mrefu kwa sababu Kocha Mokwena tangu ameingia pale amekuwa akihitaji mshambuliaji na chaguo lake la kwanza ni Mzize.
.
Mokwena ni shabiki sana wa Mzize, mimi nazungumza nae na ananiambia anamtaka Mzize awe nae hata kama sio Wydad basi kwenye timu nyingine atakayokuwepo. Kwa hiyo ni kweli wanamuhitaji na waliongea na Rais wa Yanga [Eng. Hersi Said] akawajibu kuwa anataka Mzize abaki Yanga hadi atakapomaliza msimu.
.
Mzize mwenyewe karidhia hataki kuondoka kwa fujo. Akimaliza msimu tutakaa mezani na kuangalia kama itakuwa Wydad, England, Saud Arabia au Afrika Kusini. Tutajadili ofa zote itakayokuwa na maslahi kwa mchezaji basi Yanga itamruhusu mchezaji aende mbele.
.
— JASMINE RAZACK, MSIMAMIZI WA MZIZE

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad