Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limethibitisha kuwapoteza Askari wake wawili na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya mfululizo katika maeneo ya SAKE na GOMA yaliyofanywa na Waasi wa M23 January 24 na 28, 2025.
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano JWTZ, Kanali Gaudentius Ilonda amesema Majeruhi kwa sasa wanaendelea kupatiwa matibabu mjini Goma na taratibu za kuisafirisha milli ya Marehemu pamoja na majeruhi waliotokana na mapigano hayo zinaendelea kupitia Sekretarieti ya SADC.
“Vikundi vyetu vilivyopo nchini DRC vipo salama, imara na vinaendelea kutekeleza majukumu yake kwa maelekezo ya Uongozi wa SADC” ameeleza Kanali Ilonda.