WAPINZANI wa Simba Sc kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), Al Masry, wamethibitisha kuachana na kocha wao Ali Maher ikiwa ni siku chache baada ya droo ya robo fainali ambapo miamba hiyo ya Misri ilipangwa dhidi ya Simba Sc.
Al Masry inatarajia kumtangaza kocha mpya ambaye atakuwa na kibarua cha kuivusha klabu hiyo ya Misri kwenye hatua ya robo fainali CAFCC, wakianzia nyumbani kisha kumalizia mchezo wa mkondo wa pili jijini Dar es Salaam mwezi Aprili.