Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na TCRA na Benki ya Tanzania wamefanikiwa kuwakamata Watu 12 kwa tuhuma za kujihusiha na utapeli Kwa njia ya mtandao kupitia kampuni ya inayofahamika kwa jina la LEO BENETH LONDON maaruku kama LBL .
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro SACP Alex Mkama amesema Watu hao wamekamatwa wakiwashawishi Watu kujiunga na kampuni hiyo inayoendesha biashara hiyo mtandaoni bila ya kuwa na kibali kutoka Benki Kuu jambo ambalo ni kosa kisheria ambapo baadhi yao wamekutwa na Vijana zaidi ya 100 wakiwa wamewafungia ndani na kuwapa elimu namna ya kufanya biashara hiyo kwa madai ya kuwapa ajira.
Amesema biashara hiyo inachezwa mtandaoni ambapo Watu wanatakiwa kutazama video fupi ndipo wapate fedha ambapo wanatakiwa kutoa kiingilio kuanzia Tsh. 50,000, laki 1.5 na Tsh. 540,000 na kwamba baadhi ya Watuhumiwa wamekutwa tayari wamechukua Tsh. milioni 20 ambazo tayari zipo mtandaoni na kuwaahidi kuwa watakuwa Mabilionea.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia Watuhumiwa watano akiwemo Gerald Masanya (31) Meneja wa Kampuni ya LBL Mbeya, Mkazi wa Nsalaga, Saphina Mwamwezi (23) Sekretari, Mkazi wa Ituha, Edda William (29) Mkazi wa Uwanja wa Ndege wa Zamani, Yohana Mkinda (29) Mkazi wa Tukuyu na Macrine Sinkala (23) Mkazi wa Nsalaga kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyohiyo ya upatu mtandaoni bila kuwa na kibali wakitumia kampuni iitwayo LBL MBEYA MEDIA LIMITED.