Wazazi Waishtaki TIK TOK Kufuatia Vifo vya Watoto Wao

Wazazi Waishtaki TIK TOK Kufuatia Vifo vya Watoto Wao


Wazazi wa vijana wanne wa Uingereza wameishtaki TikTok kwa madai kuwa vifo vya watoto wao vilisababishwa na changamoto (CHALLENFGE) hatari ya mtandaoni inayojulikana kama #blackoutchallenge.


Kesi hiyo imewasilishwa na #SocialMediaVictimsLawCenter nchini Marekani dhidi ya TikTok na kampuni mama, ByteDance. Wazazi wanadai kuwa usambazaji mudhui wa TikTok uliwalenga watoto wao kwa maudhui hatari ili kuongeza muda wao wa matumizi ya programu hiyo na kuongeza mapato ya kampuni.


#TikTok imesema kuwa imekuwa ikizuia video na hashtag zinazohusiana na changamoto hiyo tangu mwaka 2020 na inajitahidi kuondoa maudhui hatari kabla hayajaripotiwa.


Kesi hii inakuja wakati ambapo sheria mpya za #OnlineSafetyAct nchini Uingereza zinawataka watoa huduma za mitandao ya kijamii kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya changamoto hatari na maudhui yenye madhara makubwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad