Web

Wema Sepetu, Gigy Money Wakoshwa na Pacome

Wema Sepetu, Gigy Money Wakoshwa na Pacome


NYOTA wa Yanga raia wa Ivory Coast, Pacôme Zouzoua kazua balaa jipya kwa wasanii wa kike wa Bongo Fleva na Bongo Movie ikiwa ni siku chache tu tangu Stephanie Aziz Ki kuangukia kwa mjasiriamali, Hamisa Mobetto na kuamua kufunga ndoa.


Pacome amekuwa na ushawishi mkubwa kwa wanawake wengi mjini na baadhi kuzushiwa kutoka naye kimapenzi huku wakikataa na kudai ni marafiki tu, lakini kwa kinachoendelea haitashangaza yakitokea kama yaliyotokea kwa Aziz Ki.


"Mimi ni shabiki wa Yanga, japo siwezi taja majina ya timu zote sababu siwafuatilii sana, ila ukiniuliza mchezaji gani ananikosha akiwa uwanjani nitakwambia Pacome. Napenda jinsi anavyojituma uwanjani, yaani anapambana, pia anamuonekano mzuri hata akiwa nje ya uwanja, ukimuangalia tu, unasema yes huyu ni bonge la mchezaji."amesmema Wema Sepetu


"Yule Pacome Zouzoua namzimikia sana, kwanza mimi sijui mpira ila nikisikia siku Yanga inacheza, basi namwangalia Pacome tu atafanya nini uwanjani. Yule bana ana kitu halafu smart boy na anajua wajibu wake, we angalia vizuri jina lake linavyowika ukiona hivyo basi ana kazi nzuri uwanjani, mie nampenda sana." amesema Gigy Money

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad