Jeshi la Polisi Mkoani Geita linawashikilia Watu saba wanaotuhumiwa kujihusisha na kampuni ya biashara ya fedha mtandaoni huku wakitumia video fupi katika kutapeli Wananchi Wilayani Geita Mkoani Geita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita , Adam Maro amesema “Jeshi la polisi Mkoani Geita limeendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa Raia na mali zao kuanzia February 18,2025 kwa kushirikiana na vyombo vya usalama, tumefanikiwa kupata taarifa za uwepo wa kampuni ya LBL ambayo ipo eneo la Katoro na kuwakamata Watu saba wanaojihusisha na kampuni hiyo ambayo imekuwa ikiwatoza Wananchi vingilio vya Tsh. 50000, Laki 1.5 na Tsh.540000”
Watuhumiwa hao ni Juma Nickolaus Lukanura , Stephano Mkafulila , Ramadhani Masud , Alfred Matini , Rebeka Mazabari , Elizabeth Zacharia na Athuman Masud na wote wanatarajia kufikishwa Mahakamani.