Shughuli imemalizika katika dimba la KMC Complex, Wananchi wakiendelea kujitanua zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Singida Black Stars.
Yanga Sc imesogea mpaka alama tano mbele ya Simba Sc iliyopo nafasi ya pili wakifikisha pointi 52 baada ya mechi 20 ingawa wamecheza mechi mbili zaidi ya Mnyama.
FT: Yanga Sc 2-1 Singida Black Stars
⚽ 15’ Mzize
⚽ 44’ Dube
⚽ 90+3’ Sowah