Yanga Yamtwanga 4 Bila Kagera Sugar, Yakwea Kileleni....



Timu ya #Yanga imepata ushindi wa Magoli 4-0 dhidi ya #KageraSugar kwenye Uwanja wa KMC, matokeo ambayo yanaipeleka kileleni katika Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi 42 huku Kagera ikibaki nafasi ya pili kutoka chini (15) ikiwa na alama 11

‘Waliocheka na nyavu’ katika mchezo huo ni Clement Mzize dakika ya 32, Mudathir Yahya (60), Pacome Zouzoua (77) na Kennedy Musonda (86)

Yanga ambayo imecheza michezo 16 ipo mbele ya Timu ya #Simba ambayo ina pointi 40 katika michezo 15

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad