Web

Zidane Sereri Mdogo Mwenye Kiu ya Mafanikio Kisoka

 Zidane Sereri @zidane_723, kijana mdogo mwenye kiu ya mafanikio ya kisoka, ameendelea kuthibitisha thamani yake ndani ya kikosi cha Azam FC. Katika mchezo mgumu dhidi ya Simba SC, Sereri aliibuka shujaa kwa Azam FC baada ya kufunga bao la kusawazisha katika dakika za jioni, akitokea benchi na kuonesha kuwa yeye ni supersub wa kiwango cha juu.


Zidane Sereri Mdogo Mwenye Kiu ya Mafanikio Kisoka

Kama jina lake linavyobeba uzito wa mpira wa miguu, Zidane Sereri ameonesha kuwa si tu anaitwa Zidane kwa bahati, bali kipaji chake kinasimama imara uwanjani. Kasi yake, maarifa ya mpira, na ujasiri wa kushambulia vimeendelea kumlipa, huku akionesha kwanini mabosi wa Azam FC, akiwemo CEO abdulkarim.amin Popat , walifanya uamuzi sahihi wa kumsajili.

Hakuna shaka kuwa Sereri ni mmoja wa wachezaji wa kizazi kipya wenye mustakabali mzuri. Mbinu zake za kushambulia na maamuzi sahihi anapokuwa na mpira vimeanza kumfanya kuwa jina kubwa kwenye soka la Tanzania. Jana, Uwanja wa Mkapa ulitambua uwepo wake, na mashabiki walilazimika kukubali kuwa dogo ni hatari!

Kama alivyowahi kusema Arsène Wenger:

"Wachezaji wenye vipaji wanahitaji nafasi ya kuonesha uwezo wao. Kitu cha msingi ni kuwa na imani nao na kuwapa mazingira sahihi ya kukua."


Na kwaZidane Sereri, future is bright! Kila mchezo unaofuata, macho yataendelea kumwangalia, na bila shaka, ataendelea kuthibitisha kuwa yeye ni nyota wa kesho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad