Wanandoa Mitchell na Jennifer wamesema abiria alifariki ndani ya ndege ya Qatar Airways iliyokuwa ikitoka Melbourne kwenda Doha, na kwakuwa alikuwa na mwili mkubwa kuhamishwa, wahudumu walilazimika kumlaza kwenye kiti karibu na Mitchell kwa saa nne.
Wanandoa hao wamelalamika kuwa tukio hilo lilikuwa la kushtua, hasa kwa sababu hakuhamishwa licha ya kuwepo viti vilivyo wazi.
Qatar Airways imejibu kuwa wahudumu walifuata taratibu sahihi na walijaribu kuwahamisha abiria waliokuwa karibu, na mmoja wao kukaa na mwili wa marehemu hadi walipotua Doha.