Web

Ajali Mbili Zaua Watu Saba Same.....

Ajali Mbili Zaua Watu Saba Same.....


Watu saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro ambapo ajali ya kwanza imetokea usiku wa kuamkia leo March 30,2025 katika maeneo ya Njoro ikihusisha basi la Kampuni ya Osaka lililokuwa likielekea Dar es salaam na kusabiaha kifo cha Mtu mmoja na wengine 52 kujeruhiwa.

Ajali ya pili imehusisha basi aina ya Coaster ambalo limepinduka asubuhi leo katika kona za milima ya Ilamba na kusababisha vifo vya Watu sita na majeruhi 23, waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Wanakwaya waliokuwa wakisafiri kutoka Chome kuelekea Ndolwa.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, ameonesha masikitiko yake kutokana na vifo hivyo na kuwasihi Madereva kuwa waangalifu wanapopita Wilayani Same kutokana na hali ya hewa yenye upepo mkali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad