Mchambuzi wa michezo Alex Ngereza amezungumza machache kuhusu Khalid Aucho,Alex Ngereza amesema
"Yanga hawajapata mbadala sahihi wa Khalid Aucho na sidhani kama atakuwa na kiwango bora kwa msimu ujao kwasababu hata msimu huu Aucho hayupo kwenye ule ubora ambao alikuwa nao msimu uliopita kwenye baadhi ya mechi hasa zile mechi ambazo zinaonekana ngumu kwa Yanga"
"Nafikiri Yanga wanatakiwa kupata kiungo mwingine mwenye uwezo wa kuchukua nafasi yake na kutoa ubora kama ule au zaidi yake kabla hajaisha kabisa"
Je ni kweli Khalid Aucho ameshuka kiwango???