Web

Ali Kamwe Aibua Mapya, Kumbe Yanga Bado Hawajaenda Kushtaki CAS Kama ilivyoripotiwa


Ali Kamwe Aibua Mapya, Kumbe Yanga Bado Hawajaenda Kushtaki CAS Kama ilivyoripotiwa

Ali Kamwe Aibua Mapya, Kumbe Yanga Bado Hawajaenda Kushtaki CAS Kama ilivyoripotiwa


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe ameweka wazi kuwa klabu hiyo bado haijachukua uamuzi wa kwenda kwenye Mahakama ya Kimataifa Inayoshughulikia Migogoro ya Kimichezo (CAS). Hata hivyo alisema, kama klabu hiyo haitapata haki yake italazimika kufanya hivyo.


Akizungumza na waandishi wa habari Machi 28, 2025 Ali Kamwe alisema kuwa kama Yanga haitapata haki yake italazimika kwenda kwenye mamlaka za juu zaidi (CAS). Jambo ambalo limeibua ukweli ambao hapo awali haukuwa unafahamika kwa wadau wa soka.
E

Ikumbukwe kuwa, kabla ya kauli iliyotolewa na Ali Kamwe kulikuwa na taarifa kuwa, klabu ya Yanga tayari ilishawasilisha shauri lake CAS ikiomba ipewe alama tatu mara baada ya TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kufanya jambo hilo.

Ali Kamwe kupitia mahojiano hayo, alisema kuwa msimamo wa Yanga bado ni ule ule. Ambapo hata waandishi wa habari inatakiwa waondoe akilini mwao suala la Yanga kuingiza timu uwanjani endapo TFF na Bodi ya Ligi watapanga tarehe mpya ya mchezo.

Huku akiongeza kuwa msimamo wao kama Yanga utasaidia kupiga hatua moja kwenda mbele kwenye ukuaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania. Kwani wanataka kuhakikisha kuwa, kanuni za mpira nchini zinafuatwa.

Jambo ambalo limeonekana kuungwa mkono na mashabiki na wanachama wa klabu hiyo. Ambapo, hata wakati wa kikao cha viongozi wa Yanga na serikali walikuwepo nje ya uwanja wa Mkapa wakiwa na tshirt zenye ujumbe kuwa hawapo tayari kucheza tena.

Hivyo basi, mpaka sasa klabu ya Yanga bado haijaenda CAS lakini itafanya hivyo kama haitopata haki yake. Na, haipo tayari kucheza mchezo mwingine dhidi ya Simba msimu huu.

Je, una maoni gani kuhusu sakata hili mpaka sasa? Karibu kwa maoni hapo chini.

Chanzo: Wasafi Media/Opera News


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad