Watu sita wamefariki Dunia na wengine 49 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali usiku wa kuamkia leo katika eneo la Chigongwe Jijini Dodoma.
Ajali hiyo imehusisha lori na basi lenye namba za usajili T405 BYS, kampuni ya AN Classic lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiambatana na vyombo vya ulinzi na usalama alifika eneo la tukio na kusema kuwa majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma kwaajili ya kupatiwa matibabu, huku 23 kati yao wakiwa tayari wameshafanyiwa upasuaji.
Aidha, miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma, ikisubiri utambuzi.