“Bodi ya Ligi Kuu ni sehemu ya tatizo, TFF ni sehemu ya tatizo na Simba na Yanga nazo ni sehemu ya tatizo……” sehemu ya majibu ya Katibu Mkuu wa zamani wa TFF Angetile Osiah wakati akishauri nini kifanyike juu ya sakata linaloendelea baada ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba kuahirishwa.
Osiah ameshauri uchunguzi ufanyike na yeyote atakayekutwa na hatia awajibishwe kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu ili kila upande uone haki imetendeka hata mchezo huo utakapopangiwa tarahe mpya pande zote ziwe tayari kucheza bila mashaka.