Kamati ya Usimamizi na Uendesha ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza rasmi kuahirisha mchezo wa Ligi Kuu namba 184 kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC uliyopangwa kuchezwa leo saa 1:15 usiku.
Bodi imefanya maamuzi hayo baada ya kupokea taarifa ya awali ya Ofisa Usalama wa Mchezo ambayo imeanisha matukio kadhaa yaliyopekea Simba SC kushtaki kwa TFF na Bodi ya Ligi kutokana na kushindwa kufanya mazoezi.
Bodi ya Ligi imesema mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusiana na sababu zilizosababisha mchezo huo kutochezwa.