Web

Bondia Mwakinyo Adaiwa Kujeruhi Kwa Kisu na Mbwa Tanga




Kijana aliyefahamika kwa jina la Mussa Ally mkazi wa Sahare, Jijini Tanga amemtuhumu Bondia wa Ngumi nchini, Hassan Mwakinyo Kumshambulia kwa kisu, na kumfungulia mbwa wanne Majira ya saa 12 Alfajiri alipokuwa akiokota nazi zilizokuwepo barabarani katika mtaa wa Sahare Vijijini

Akiongea kwa Maumivu ya Majeraha hayo akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo, Mussa amesema aliamka asubuhi kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zake za kila siku, na alipokuwa njiani alikutana na nazi ambazo akaanza kuziokota.

Amesema wakati anaziokota, Hassan Mwakinyo alifika akiwa na Kijana wake wa Kazi ambaye alimuuliza Nazi umetoa wapi? Na kujibu ameziokota barabarani, ambapo Mwakinyo alimjibu umeyakanya na kuanza kumshambulia kwa kumpiga mtama na kumburuza nyumba kwake.

Mussa amedai kuwa wakati Mwakinyo akiendelea kumshambulia, akamuagiza kijana wa kazi kisu na kuanza kumkata miguu na kumvua nguo na kufungulia mbwa waliokuwa wakimjeruhi kwa zaidi ya lisaa limoja

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad