BREAKING: Kesho ni Sikukuu ya EID, Mufti Atangaza
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ametangaza kuwa mwezi umeonekana katika maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani hivyo kesho Jumatatu March 31,2025 itakuwa ni Sikukuu ya Eid Al Fitri.
Akitangaza Jijini Dar es salaam leo, Mufti Zubeir amesema “Nawatangazia Waislamu wote kuwa mwezi umeandama na umeonekana na kushuhudiwa sehemu nyingi katika nchi yetu, pia umeonekana Kenya, Pemba na Arusha wameona waziwazi mwezi, hivyo nimeuthibitisha mwezi huo na kesho itakuwa Eid”