Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetangaza ratiba mpya ya robo fainali za michuano yake mikubwa, Ligi ya Mabingwa ya CAF na Kombe la Shirikisho la CAF, kwa msimu wa 2024/2025. Taarifa hii ilitolewa leo, Machi 23, 2025, na imeleta shauku kubwa miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka barani Afrika.
Ratiba ya Robo Fainali za Ligi ya Mabingwa ya CAF:
Mechi za Mkonzo wa Kwanza:
Jumanne, Aprili 1, 2025:Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs. Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) saa 13:00 GMT.
Al Ahly SC (Misri) vs. Al Hilal SC (Sudan) saa 21:00 GMT.
Pyramids FC (Misri) vs. AS FAR (Morocco) saa 21:00 GMT.
MC Alger (Algeria) vs. Orlando Pirates (Afrika Kusini) saa 21:00 GMT.
Mechi za Mkonzo wa Pili:
Jumanne, Aprili 8, 2025:Al Hilal SC vs. Al Ahly SC saa 21:00 GMT.
AS FAR vs. Pyramids FC saa 21:00 GMT.
Esperance Sportive de Tunis vs. Mamelodi Sundowns saa 21:00 GMT.
Jumatano, Aprili 9, 2025:Orlando Pirates vs. MC Alger saa 19:00 GMT.
Ratiba ya Robo Fainali za Kombe la Shirikisho la CAF:
Mechi za Mkonzo wa Kwanza:
Jumatano, Aprili 2, 2025:Stellenbosch FC (Afrika Kusini) vs. Zamalek SC (Misri) saa 13:00 GMT.
Asec Mimosas (Côte d'Ivoire) vs. RS Berkane (Morocco) saa 19:00 GMT.
CS Constantine (Algeria) vs. USM Alger (Algeria) saa 19:00 GMT.
Al-Masry SC (Misri) vs. Simba SC (Tanzania) saa 19:00 GMT.
Mechi za Mkonzo wa Pili:
Jumatano, Aprili 9, 2025:Simba SC vs. Al-Masry SC saa 16:00 GMT.
Zamalek SC vs. Stellenbosch FC saa 19:00 GMT.
RS Berkane vs. Asec Mimosas saa 21:00 GMT.
USM Alger vs. CS Constantine saa 21:00 GMT.
Kwa upande wa Simba SC, timu ya Tanzania, itakutana na Al-Masry SC ya Misri katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF. Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa tarehe 2 Aprili 2025 huko Misri, na marudiano yanatarajiwa kufanyika tarehe 9 Aprili 2025 jijini Dar es Salaam.