Web

Dabi ya Kariakoo, Kocha Shungu Amtaja Ikangalomba, Amtoa Hofu Kocha Yanga



Kocha msaidizi wa AS Vita, Raoul Shungu aliyotoka Ikanga Speed amemuondoa wasiwasi Hamdi akisema hatashangaa kuona winga huyo anafanya kitu kikubwa kama atacheza dhidi ya Simba.

Shungu ambaye amewahi kufanya kazi Yanga, alisema Ikanga Speed ni mchezaji mkubwa aliyecheza mechi kubwa za watani wa jadi na kwamba anavyowajua mashabiki wa Yanga wanavyojaa uwanjani kama winga huyo atapata nafasi atafanya kitu tofauti.

“Nimeona amecheza mechi iliyopita, nilisikia alitakiwa kupunguza uzito, inawezekana kwa kuwa hapa alisimama kucheza kwa muda wakati analazimisha kuondoka, lakini nimemuona amerudi kwenye mwili wake,” amesema Shungu.

“Kama kocha wa Yanga hapo atampa muda wa kucheza dhidi ya Simba atafanya vizuri sana, nadhani mashabiki wa Yanga wataona ubora wake na kama wakijaa vizuri uwanjani hilo ndio wachezaji Wakongomani wanataka atajituma sana kufanya mambo makubwa."

Ikanga Speed alitua Yanga kupitia dirisha dogo na alikuwa hajatumika kwa mchezo wowote tangu enzi za kocha Sead Ramovic na hata alipokuja Hamdi ambaye alimpa dakika 21 dhidi ya Pamba Jiji na kukata kiu ya mashabiki wa timu hiyo waliokuwa na hamu ya kumuona uwanjani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad