Web

Donald Trump Aipa Hamas Onyo la Mwisho Waachieni Mateka Mara Moja

Donald Trump Aipa Hamas Onyo la Mwisho Waachieni Mateka Mara Moja


Rais wa Marekani Donald Trump ametoa kile alichokiita “onyo la mwisho” kwa Hamas kuwaachilia mara moja mateka wote walioko Gaza – hatua iliyokuja saa chache baada ya Ikulu ya White House kuthibitisha kuwa ilikuwa ikifanya mazungumzo moja kwa moja na kundi hilo la wanamgambo.

“Waachilie mateka wote sasa, si baadaye, na urejeshe mara moja miili yote ya watu uliowaua, la sivyo itakuwa MWISHO kwenu,” Trump aliandika kwenye Truth Social Jumatano, muda mfupi baada ya kukutana na mateka wanane waliokuwa wameachiliwa katika Ikulu ya White House.

Trump aliandika kuwa ataitumia Israeli “kila kitu inachohitaji ili kumaliza kazi,” na akaonya kwamba “Hakuna mshiriki hata mmoja wa Hamas atakayekuwa salama ikiwa hamtafanya ninavyosema.”

Maoni hayo yalitolewa saa chache baada ya Marekani kuthibitisha ripoti kwamba ilikuwa ikifanya mazungumzo moja kwa moja na Hamas kuhusu mateka na usitishaji mapigano huko Gaza, hatua inayokwenda kinyume na jadi yake ya kutozungumza na makundi inayoyachukulia kuwa mashirika ya kigaidi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad