Web

Dunia Kushuhudia Vifo zaidi Vikitokana na Ugonjwa wa Ukimwi

Top Post Ad

Dunia Kushuhudia Vifo zaidi Vikitokana na Ugonjwa wa Ukimwi


Kunaweza kuwa na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) 2,000 kila siku kote ulimwenguni kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili wa Shirika la misaada la M arekani (USAID). Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS) lilisema siku ya Jumatatu.

"Iwapo msaada wa Marekani hautarejeshwa na hautabadilishwa na ufadhili mwingine na hatujasikia kuhusu serikali nyingine zikiahidi kuziba pengo hilo, kutakuwa na vifo vya ziada vya UKIMWI milioni 6.3 katika miaka minne ijayo," alisema Winnie Byanyima, mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva siku ya Jumatatu.

Hata hivyo, usumbufu katika ufadhili wa huduma za afya na athari kwa huduma zingine ulikuwa na madhara makubwa kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI, alisema Byanyima.

"Kusitishwa ghafla kwa ufadhili wa Marekani kumepelekea kufungwa kwa kliniki nyingi, kupoteza maelfu ya wafanyakazi wa afya... Yote haya yanamaanisha kuwa tunatarajia kuona ongezeko kubwa la maambukizi mapya ya Ukimwi.

UNAIDS imekadiria kuwa tunaweza kuona maambukizi mapya 2,000 kila siku," alisema. Byanyima alisema takwimu hizo zilikuwa msingi wa mifano ya Umoja wa Mataifa, lakini hakutoa maelezo zaidi juu ya jinsi makadirio hayo yalivyofikiwa.

Ujumbe wa Marekani mjini Geneva haukujibu mara moja ombi la kutoa maoni yake kutoka kwa Reuters.

Byanyima alisema kwamba ikiwa ufadhili kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) hautaendelea baada ya kusitishwa kwa muda wa siku 90, kufikia Aprili, au hautabadilishwa na serikali nyingine, "basi kutakuwa na vifo vya ziada vya UKIMWI milioni 6.3 katika miaka minne ijayo."

Kwa mujibu wa data za hivi karibuni, kulikuwa na vifo 600,000 vinavyohusiana na UKIMWI duniani kote mwaka 2023, aliongeza. "Kwa hiyo tunazungumzia ongezeko la mara kumi zaidi."

Utawala wa Trump umesema kuwa ufadhili huo ulisimaishwa ili kuhakikisha kuwa unakwenda sawa na sera yake ya "America First" (Marekani Kwanza).

 


Below Post Ad

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.