Ellie Mpanzu na Jonathan Ikangalombo wote walikuwa kwenye kikosi cha Vitta Club pale Congo lakini Mpanzu alianza kuondoka baadaye Ikangalombo akafuata,
Wakati anaingia Yanga Sead Ramovic alisema jamaa ni mzito sana ndiyo maana hakumtukia kwenye michezo yake ya mwanzoni,
Hivi sasa mchezo wake wa 3+ miongoni mwa michezo yake ni miwili rasmi Vs Pamba, Vs Songea na ule wa kirafiki dhidi ya Singida Black Stars.
Kama utakumbuka niliwahi kusema Ikangalombo hawezi kukosa namba Yanga licha ya timu kuwa na wachezaji bora wengi kwenye nafasi yake kwa nini?
Ngoja nikurejeshe fainal za Chan 2022 Congo iliishia hatua ya makundi ikiwa na mastar kibao kama Boka,Max, Mpian na Mpanzu
Ikangalombo kwenye michuano ile alichukua tuzo ya mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast ambayo beki wao aliyekuwa anamkaba Ikangalombo alikuwa Yao huyu wa Yanga.
Alichukua tuzo pia kwenye mechi dhidi ya Uganda kumbuka mechi mbili mfululizo Congo inatoa sare yeye akiendelea kuwa hatari. mchezo mmoja tu dhidi ya Senegal hapa Congo walikula chuma 3 hii alikosa tuzo ila aliimbwa sana.
Huyu Ikangalombo amecheza timu mbili bora za Congo kwanza DC Motemapembe klabu iliyo mtambulisha hii ndiyo klabu namba tatu kwa ubora Congo,
Baadaye akajiunga Vitta Club licha ya kuwa hakupata sana mafanikio sio tu ya timu kiujumla lakini hata yake mwenyewe tuzo binafsi lakini alicheza na wachezaji bora.
Huku Yanga Ikangalombo ameanza na mwanzo mzuri baada ya kuonekana kufunga kwa sababu timu zote mbili alizopita hata timu ya taifa hakuwa sana akifunga magoli licha ya uhatari wake.
Ikangalombo huyu ni kiungo mshambuliaji anaweza kutokea katikati ama pembeni ana kasi kubwa ya kukokota mpira anapiga krosi na kufunga
Kama Miloud Hamdi atamtumia kwenye kutengeneza zaidi nadhani Yanga watanufaika nae zaidi kuliko DC Motemapembe ama Vitta Club.