Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Steven Mguto katika mahojiano yake na Kituo cha Habari cha Mwananchi Digital amesema iwapo wao Kama mamlaka za kimpira watashindwa kutatua sakata la Simba na Yanga kuhusiana na mechi Yao iliyoshindikana kupigwa Machi 8, 2025 basi wataishirikisha Serikali.
Hayo yamejiri baada ya bodi kuahirisha mchezo huo wa Derby ya Kariakoo na Yanga kuandika barua ya kubainisha kuwa hawataucheza tena mchezo huo na kudai alama tatu.
“Jambo hili likitushinda kabisa lazima tuihusishe Serikali iweze kusaidia, kwasababu kuhakikisha amani inakuwepo sio suala letu sisi peke yetu kila mtu anatakiwa kuhakikisha kuna kuwa na amani,” amesema Mguto.