Rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon Samuel Eto’o ameshinda kesi yake katika mahakama ya usuluhishi wa michezo y CAS dhidi ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Samuel Eto’o ameshinda kesi hiyo baada ya Mahakama ya usuluhishi wa michezo (CAS) kutoa uamuzi uliomuunga mkono na kumfanya kuwa mgombea tena katika uchaguzi ujao wa CAF.
Baada ya uamuzi huo wa CAS, sasa CAF itatakiwa kumlipa Etoo Faranga 8000 za Uswizi na kutakiwa kurejeshwa katika orodha ya wagombea wa urais CAF zikiwa zimebaki siku 5 pekee tu kuelekea uchaguzi.
Hukumu hiyo, imeyotolewa leo Machi 7, 2025, huko Lausanne nchini Uswisi, na kusafisha njia kwa Eto’o na shirikisho la soka la Cameroon (FECAFOOT), ambalo lilipinga kutengwa kwake kwenye kinyang’anyiro hicho.