Ukipitia #Comments nyingi baada ya Gigy Money kuachia ngoma yake mpya #Nimenasa aliyomshirikisha Mkongwe TID utaona Watu wengi wanashauri Gigy aachane na Muziki kwani hana sauti nzuri, hajui kuimba, kiufupi anapenda Muziki ila Muziki haumpendi. Wengi wamefikia mpaka hatua ya kusema bora Rose Ndauka ana Idea ya Muziki ila sio Gigy Money.
Kiukweli lazima tu-set Standard ya Muziki wetu wa Bongo Fleva kama kila mtu ataamua kuwa Mwanamuziki na Kuimba ngoma mbovu basi muziki wetu hautaenda popote, naamini Media nyingi za Bongo huenda zikatoa #Airtime kwa wimbo lakini kuna ngoma kali za Wasanii Wachanga hazipewi nafasi kisa tu hawana majina makubwa kama Gigy Money.
Producer wa Ngoma hii alikubali vipi itoke au ndio njaa na kumsikiliza tu Gigy bila kumkosoa na kumshauri akafanye kazi nyingine maana muziki hawezi!, Pia TID amekubali vipi Collabo, haoni kama anashusha hadhi yake aliyoijenga kwa Muda mrefu? wengi tunaelewa kuwa TID anaimba kinoma ni mkali wa Live Performance, inakuaje anafanya Collabo na Gigy na ameshindwa kumbadili Gigy angalau aimbe Vizuri ngoma iwe kali?
Bongo tukiendelea Kuchekea chekea Wasanii kama Gigy basi muziki wetu kufika International tutasubiri sana, Gigy ana mashabiki wengi huenda Watoto wanaomuoana Kama Mfano wao wakaamini kuwa nyimbo zake ni nzuri hivyo na wao watamuiga na hapo tutakuwa tunatengeneza kizazi cha hovyo kisichojua muziki.
Naamini Gigy ana mambo mengi tu yanayomuingizia hela, akomae nayo, mambo ya muziki aachie wenye Talent, ngoma zake kiukweli hazivutii. NAMKUBALI SANA GIGY LAKINI KWENYE MUZIKI ATUPISHE.
#hopetygatz