Web

Haji Manara Aanzisha Kampeni ya "Karia Must Go"



Baada ya kusambaa kwa video jongefu ikimuonesha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, akizungumza wakati wa Iftar iliyoandaliwa na shirikisho hilo jijini Tanga, mjadala mkubwa umeibuka. Katika video hiyo, Karia anasikika akisema:

"Tutakuwa tunaongea na waandishi wa habari, tuwape yote haya kwenye media zetu zilizoko Tanga, maana yake hizo media zingine zimechafuka, zina mambo yao yale."

Kauli hiyo imeibua mjadala mkali, hususan kutoka kwa Mwanachama wa Yanga, @hajismanara , ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameonesha kutoridhishwa na kauli ya Karia.

Katika ujumbe wake, Manara ameandika:

"Hizo media nyingine unazosema zimechafuka ndizo hizo hizo huzitumia kuhamasisha soka ya nchi hii, na ndizo zilizokutambulisha kwa jamii. Unachofanya ni ubaguzi wa wazi wazi kama kiongozi mkuu wa soka nchini, na kwa hili umeshapoteza uhalali wa kuendelea kuongoza TFF.

Manara ameendelea kudai kuwa Rais huyo wa TFF amepoteza sifa za kuendelea kuongoza shirikisho hilo.

"Sioni tena kama unastahili kubaki kwenye shirikisho kama kiongozi. Umeleta ukanda na umedharau media nyingine za nje ya mkoa wa Tanga! Kiburi na majivuno yako yamevuka mpaka. Kiukweli, jamaa he is too drunk in power to be sober."

Aidha, Manara amedai kuwa Karia anazua migogoro kati ya vyombo vya habari vya Tanga na vile vya nje ya mkoa huo. Ameendelea kumshutumu kwa kile alichokiita "kutafuta huruma" kwa kutumia jukwaa la Iftar.

"Bora ungenyamaza tu kipindi hiki kuliko kwenda kutafuta sympathy Tanga na kuwatumia watu wakusifu hadi kwenye majukwaa ya Iftar. Haikusaidii hata kidogo, kwa sababu hata waliokuwa wakikuunga mkono wameshaona sura yako halisi!"

Katika hitimisho lake, Manara amependekeza kuwa Karia apishe nafasi hiyo na kuachia makamu wake akaimu urais wa TFF hadi uchaguzi ujao mwaka 2026.

Hadi sasa, kauli za Karia zimeendelea kuzua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii huku Manara akiwataka wanayanga kuanza kampeni ya KariaMustGo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad