Web

Haji Manara Hataki Utani, Aweka Wazi Kumburuza Maimartha Jesse Mahakamani




Mwanamitandao mashuhuri nchini Tanzania, Haji Manara ameweka wazi kuwa yupo mbioni kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mwanahabari, Maimartha Jesse wa Mai TV. Hii ni baada ya mwanahabari huyo kuanika taarifa kuhusu ndoa ya Manara na Zaiylissa.



Kupitia mtandao wa Instagram katika ukurasa wake, Alhamisi ya Machi 6, 2025 Manara aliweka wazi kuwa hawezi kuvumilia kile kinachoendelea kufanywa na mwanahabari, Maimartha Jesse ambaye ni mmiliki wa kituo cha habari za mitandaoni nchini, Mai TV.

Hii ni baada ya Maimartha Jesse kuanika taarifa kuwa ndoa ya Manara na Zaiylissa imeshavunjika. Jambo ambalo inasemekana kuwa halikuwa na ukweli wowote kwa kuwa wanandoa hao wanaonekana kuwa pamoja.



Baada ya kutoa taarifa hiyo, Maimartha Jesse alienda mbali zaidi kwa kuufahamisha umma kuwa Manara yupo mbioni kuoa mke wa pili. Huku akidai kuwa kitu hicho kimepingwa na Zaiylissa ambaye ni mke halali wa Manara.



Jambo ambalo limemuibua Manara huku akisema kuwa Maimartha anapotosha umma. Kwani vyote anavyoviongea kuhusu ndoa yake ni vya uongo. Kitu kinachomfanya atilie mashaka taaluma ya Maimartha kwa kudai kuwa amejikita zaidi kwenye kudhalilisha.



Kupitia chapisho hilo, Manara amesema kuwa anataka kumfanya Maimartha Jesse kuwa mtu wa mfano kwa watu wengine wenye tabia kama zile. Kwani hafurahishwi na kitendo cha watu maarufu kuchafuliwa kwenye mitandao.



Jambo linaloonesha wazi kuwa amechoshwa na tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa zao uongo. Ndiyo maana anataka kumfikisha kwenye vyombo vya sheria ilikusudi apate funzo, kitu kitakachomfanya abadilike.

Manara ameenda mbali zaidi kwa kusema kuna anaona kila dalili ya Maimartha kuachana na kazi ya kuchapisha habari za uongo kuhusu watu. Ambapo anaamini kuwa atakuwa mtu wa kawaida tu, si mwanahabari.



Huku akiongeza kuwa inatakiwa ajipange kwenda kuthibitisha taarifa alizokuwa anazisambaza kuhusu ndoa ya Manara. Kwani anaamini kuwa inatakiwa kuwe na mipaka pasipo kusahau ukweli wa taarifa husika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad