Web

Hatimaye Dereva Aliyesababisha Ajali iliyomuua Kamanda Chiko Akamatwa Mbeya


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limemkamata Elia Asule Mbugi maarufu Dogo Bata (25) Mkazi wa Segerea, Dereva aliyekuwa akiendesha gari namba T 580 EAE aina TATA (daladala) ambaye alitoroka March 17, 2025 mara baada ya kusababisha ajali iliyosababisha kifo cha SP Awadh Ramadhani Chico aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro, amesema@Mtuhumiwa huyo alikamatwa na Makachero wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam March 27, 2025 huko maeneo ya Mbalizi Mkoani Mbeya na atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo.

OCD Chico alifariki March 17,2025 katika ajali ya gari akiwa anaelekea kazini katika barabara ya 33 Nyerere maeneo ya Pugu mwisho wa lami, baada ya gari lake kugongana na daladala ambapo alizikwa March 18, 2025 katika makaburi ya Kisutu Ilala Jijini Dar es salaam.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad