Web

HATIMAYE Serikali yawaita kikao TFF, TPLB, Yanga, Simba kuhusu Dabi

Top Post Ad

Serikali yawaita kikao TFF, TPLB, Yanga, Simba kuhusu Dabi


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la nchini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.

"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Ofisa mmoja kutoka bodi ya ligi pia alithibitisha kupokea kutoka sekalini kuhusu kikao hicho; "Tumefahamishwa kuhusu kikao hicho na tutahudhuria. Ajenda kuu ni mjadala unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba," alisema ofisa huyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi.

Msigwa pia alieleza maafisa wa Simba watashiriki katika kikao hicho.

Yanga imelipeleka rasmi suala hili katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) baada ya kutoridhishwa na jambo hilo.

Mchezo huo, ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Machi 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, uliahirishwa baada ya Simba kudai makomandoo wa Yanga waliwakatalia kuingia uwanjani kwa ajili ya mazoezi yao ya kabla ya mchezo.

Simba ilitoa taarifa rasmi kwa Bodi ya Ligi Kuu na TFF, haitoshiriki mchezo huo kwa sababu haki yao ya kufanya mazoezi kabla ya mechi ilikuwa imekiukwa, kama ilivyobainishwa katika kanuni za bodi ya ligi. Kwa upande mwingine, Yanga ilisisitiza mchezo huo ungechezwa kama ilivyopangwa, kulingana na kanuni za ligi.

Hata hivyo, baadaye mchana, bodi ya ligi ilitoa tamko rasmi ikitaja wasiwasi wa Simba na kutaja Kipengele cha 34.1 (1.3) cha kanuni kinachotoa ruhusa ya kuahirisha michezo kwa mazingira ya dharura.

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.