Web

Hawa Hapa Makocha Watatu Ambao Hawajaondoka ama Kufukuzwa Hadi Sasa Ligi Kuu

Top Post Ad

Hawa Hapa Makocha Watatu Ambao Hawajaondoka ama Kufukuzwa Hadi Sasa Ligi Kuu


TANGU msimu huu umeanza, ni makocha watatu tu ambao hawajaondoka au kufukuzwa hadi sasa na timu wanazozifundisha kati ya 16, za Ligi Kuu, ambapo ni Fadlu Davids wa Simba, Ahmad Ally (JKT Tanzania) na Mecky Maxime anayeifundisha Dodoma Jiji.

Fadlu ameiongoza Simba katika michezo 22, akishinda 18, sare mitatu na kupoteza mmoja akishika nafasi ya pili na pointi 57, huku Ahmad Ally akiiongoza JKT kushinda mechi saba, sare tisa na kupoteza saba, akiwa nafasi ya sita na pointi 30.

Kwa upande wa Mecky Maxime aliyechapwa mabao 6-0, dhidi ya Simba mchezo wa mwisho Machi 14, ameiongoza Dodoma kushinda michezo saba, sare sita na kupoteza 10, huku kikosi hicho kikiwa katika nafasi ya nane na pointi 27, baada ya mechi 23.

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.