Web

Hii Ndio Maana ya Sajili ya Dirisha Dogo, Yanga na Israel Mwenda....




Wakati ambao makocha wengi wakiwa wanaamini kwenye sajili za dirisha kubwa kama sehemu ambayo wanaweza kupata wachezaji wanaowataka na wengine wakiamini sio rahisi kumpata mchezaji kwenye dirisha dogo kwasababu timu haiwezi kuachia wachezaji wake muhimu katikati ya ligi.

Lakini ndio wakati ambao viongozi wa Yanga walihitaji huduma ya ISRAEL MWENDA kwenda kutibu tatizo la full back right pale mitaa ya Twiga na Jangwani na hatimaye kwa muda mfupi tu sajili imelipa na inaonyesha why mabossi walitoa hela yao kwaajili ya ISRAEL MWENDA.

Dirisha dogo la usajili haliitaji mambo mengi sana ndio maana sio rahisi kuona timu nyingi zikifanya transfer kwenye dirisha dogo kwasababu hakuna ulazima ila kama ulazima upo lazima timu ifanye machaguo sahihi ambayo yanaweza kuleta impact kwenye timu na Yanga kwa ISRAEL MWENDA wamepatia kwa asilimia kubwa.

Naelewa ule upande wa kulia YaoYao tayari ameanza mazoezi naelewa vizuri uwepo wa bwana mdogo Kibwana Shomari lakini ongezeko la mtu kama ISRAEL MWENDA ambaye ukiacha kucheza right back ana uwezo wa kucheza hata left back inaongeza competition kwenye kikosi cha Yanga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad