IBRAHIM Hamad ‘Bacca’ wa Yanga, ndiye beki aliyefunga mabao mengi ya Ligi Kuu Bara msimu huu, akiwa na manne akifuatiwa na Hernest Malonga (Singida BS), Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Namungo FC) na Pascal Msindo wenye matatu kila mmoja.
Rekodi zinaonyesha beki aliyefunga idadi kubwa ya mabao msimu uliopita alikuwa ni Derrick Mukombozi wa Namungo FC ambaye alifunga pia manne, akiwa tayari amefikiwa na Ibrahim Hamad ‘Bacca’ wa Yanga na huenda ikavunjwa kwa michezo iliyobakia.