Mchezaji wa Klabu ya Al Masry Salah Mohsen (26), ndiye mchezaji wa kuogopwa zaidi na Simba kuelekea mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika April 2, 2025.
Vile vile ndiye mchezaji mwenye wasifu mkubwa zaidi kunako kikosi cha Klabu hiyo. Alijiunga na Al Masry akitokea Al Ahly ambapo alipata mafanikio makubwa.
Kwanza anamedali mbili (2) za Ligi ya Mabingwa Afrika, ana medali ya CAF Super Cup, pia ana medali mbili (2) za Ubingwa Ligi kuu nchini Misri.
Salah msimu huu amekuwa moto wa kuotea mbali ikiwa amehusika katika magoli nane (8) ya Al Masry kwenye EPL (amefunga saba(7) na kutoa asisti moja (1). Ameisadia klabu yake kushika nafasi ya nne (4) kwenye msimamo wa ligi akikusanya alama 30 katika michezo 17 huku wakishinda michezo minane (8) wakisare 6 na kupoteza michezo 3.