Nyota wa zamani wa timu za Singida Big Stars na sasa Namungo FC raia wa Rwanda, Meddie Kagere 'MKI4', anashikilia rekodi ya kipekee wakati anacheza Simba SC kwa mastaa wa kigeni katika Ligi Kuu Bara, ambayo hadi leo inaishi na wala haijavunjwa.
Kagere alitua Simba SC akitokea Gor Mahia ya Kenya msimu wa 2018-2019 na kufunga mabao 23 na kuipiku rekodi ya aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe ya wachezaji wa kigeni kufunga mabao mengi msimu mmoja alipofunga 21 msimu wa 2015-2016.
Msimu wa 2019- 2020, staa huyo akiwa na Simba SC pia, alifunga mabao 22 na kutetea tuzo ya mfungaji bora ikiwa pia ni rekodi kwani, haijawahi kutokea kwa mchezaji yeyote iwe mzawa au wa kigeni kuchukua tuzo ya ufungaji bora mara mbili mfululizo.