Wana-footwork nzuri mguuni wanaweza kucheza dhidi ya mshambuliaji, kukokota mpira dhidi ya namba 9, Wanaanzisha mashambulizi kwa maana ya Buld-up wenyewe, wanapiga mipira mirefu ya Counter-Attack na inafika kwa mawinga bila shida.
Lakini usiwakatae muda wanapofanya makosa ya kizembe kufungwa magoli ya mbali, Bwezi vs Yanga, Malongo Vs Simba, Zile bahati mbaya kwenye contro kuzidi uwezo kujifunga kwa mipira ya kawaida ndiyo namna yao.
Lakini kuna mwenye majibu ya nini kilicho nyuma ya Aishi Manula?, kwamba ndiyo hiyo mifumo imemuondoa kwenye njia ama kuna sababu nyingine?
Nimekaa kuzikumbuka mechi ngumu za Simba kwenye ligi ya mabingwa, nikairejea ligi kuu nimegundua kuwa labda kwa kuwa mpira wa sasa unawahitaji kina Camara, Diarra kuliko kina Manula, Kaseja it's Okey lakini.
Aishi Salumu Manula ninae mjua mimi ana miaka 7+ kwenye uzi wa Simba tangu alipo jiunga 2017 akitokea Azam fc.
Aishi huyu ameipa Simba ubingwa wa ligi mara nne (4) ameipa Simba mataji mawili ya kombe ya kombe shirikisho zamani (Asfc)
Aishi huyu ameifikisha Simba hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa tena mara mbili achana na izo za hatua nyingine
Kombe la shirikisho Africa ana robo fainali moja hapo sijazitaja tuzo zake binafsi alizo zikusanya akiwa na Simba + Azam Fc
Mlinda lango bora mara mbili zaidi wa ligi kuu, amekuwa mlinda lango bora kwa mana ya kuingia kwenye kikosi bora cha mwaka mara mbili zaidi
Unapo litaja jina la Aishi sio umzungumzie yeye kama mchezaji lakini gusia uzoefu wake ligi ya ndani na kimataifa, kwenye timu yake ya taifa ameipeleka Taifa Stars Afcon
Sasa kama ni mifumo na Falsafa zimemkataa Aishi najiuliza inamana ndiye golikipa pekee aliyebakia Africa ama vipi ??.
Ngoja niendelee kusubiri mwisho wa hii season isiyo isha.
@jemedarisaid