Web

ISRAEL Mwenda Awasha Taa Nyekundu Kwa Kibwana na Yao......




ISRAEL Mwenda alipojiunga na Yanga kwa mkopo kutoka Singida Black Stars alikumbana na changamoto ya kuzoea mazingira mapya, hasa katika utimamu wa mwili. Kwa kuwa aliingia wakati wa dirisha dogo la usajili, alilazimika kutumia wiki tatu hadi nne ili kufikia viwango vya wenzake.

Kocha wa viungo wa wakati huo, Adnan Behlulovic alichukua jukumu la kumsaidia beki huyo wa kulia ili awe tayari kwa mechi, huku Kennedy Musonda akiwa kwenye mchakato wa kurejea kutoka majeruhi.

Mwenda alianza kuonyesha uwezo katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Copco Januari, mwaka huu alipoonyesha kiwango bora cha uchezaji na kutoa asisti mbili. Baada ya kufanya vizuri katika mechi hiyo ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0, mwenyewe alijivunia kiwango bora.

“Unajua unaposajiliwa dirisha dogo muda haukusubiri unatakiwa kuonyesha kwa haraka. Nina furaha na mwanzo wangu,” anasema.

Baada ya mabadiliko ya kocha, Yanga ililazimika kumvuta Miloud Hamdi kutoka Singida Black Stars ili kumrithi Saed Ramovic aliyekwenda kufanya kazi Algeria. Katika kipindi cha mabadiliko, Mwenda aliendelea kupata nafasi kikosi cha kwanza akicheza kwa dakika 360 kwenye michezo minne mfululizo ya Ligi Kuu Bara.

Katika michezo hiyo aliisaidia Yanga kupata pointi 10 kutoka JKT Tanzania waliyotoka nayo suluhu, KMC wakaichapa 6-1, Singida BS (2-1), na Mashujaa (5-0), huku akifunga bao moja. Kiwango chake kilionyesha ni kiasi gani alikuwa na mchango kwa timu, na kufanya wengi kumzungumzia.

NINI KINAMBEBA
Mwenda ameonekana kufanya vizuri katika kupanda na kushuka, jambo ambalo limeonekana kuifanya Yanga kuwa na makali katika maeneo ya pembeni. Hii ni moja ya sifa zinazompa nafasi katika timu, ambapo anachangia ufanisi wa mashambulizi na pia kujiweka vizuri kurudi nyuma na kusaidia katika kulinda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad