Jean Charles Ahoua amefanya vizuri sana kwenye msimu wake wa kwanza, yaani kwenye moja mpaka kumi nampa 8.5
Ni ngumu kwa wachezaji wa aina yake kufiti system ya timu kwa haraka ukizangatia ndo msimu wake wa kwanza na bado mchezaji kijana miaka 23 magoli 10 assists 7, Jean ni mchezaji wa kisasa kwa nafasi yake wengi wanatengenezwa kucheza kama yeye yaani kama Robots kwa sababu vitu vingi anavyofanya uwanjani anakuwa ameishafanya kwenye uwanja wa mazoezi, penalties, set pieces kona na faulo na uwanjani anafanya vitu vingi vya msingi kwa kiungo mchezeshaji.
Jean sio mbunifu kwenye sanaa yake ya uchezaji lakini sio makosa yake, mpira wake ume base kwenye two touches unatakiwa kuwa hapa unatakiwa kuwa pale yaani anacheza kwa kufuata maelekezo ya kocha sababu mazoezini sasa hivi hakuna mchezaji anapewa uhuru wa kufanya ubunifu, mbinu ndo zinaanza halafu ujuzi unafuata.
Fadlu haonekani ku mind sana pale Jean anapo poteza mpira kwenye mechi ambazo nguvu zinahitajika sababu sio kazi yake, ni ngumu sasa hivi kupata wale namba kumi ambao wanakufanya uachame yaani wale ambao wanakufanya upende kuangalia mechi za timu husika kwa sababu mpira sasa hivi ni wa maelekezo sana.
Jean ndo mchezaji bora wa Simba kwa sasa anafanya kile ambacho ni bora kwake kukifanya.