Web

Kauli za Tumekufa Kiume Mwaka Huu Zikome, Simba Hakikisheni Mnatinga Nusu Fainali

Kauli za Tumekufa Kiume Mwaka Huu Zikome, Simba Hakikisheni Mnatinga Nusu Fainali



Ni ule msimu ambao natamani kuona Simba wakivuka Robo fainali na kutinga nusu kwenye michuano ya kimataifa.

Mara kibao Simba wamekuwa wakitolewa robo na kusema “tumekufa kiume” hizi ni kauli Za kushindwa,mwaka huu zikome na timu iwaze kutinga nusu.

Simba uzoefu wa michuano wanao,Wachezaji wazuri wanao na Kocha wanae,ni zamu Yao ya kwenda nusu.

Misimu kibao Simba walishindwa kujua njia sahihi ya kucheza mechi za mtoano,mechi nyingi Simba walitaka kupishana na wapinzani kwa umiliki mkubwa na kusahau hatua kama hizi watu wanaangalia matokeo ya mwisho siyo umiliki wa mpira,ndio maana kwenye hatua ya makundi akikutana na Al Ahly unajipigia Ila kwenye hatua Za mtoano Al Ahly anakuachia mpira na kupiga counter attack….yeye anajali matokeo ya mwisho siyo umiliki.

Fadlu anatakiwa kucheza kama Pele,lazima ajue hii ni hatua ya mtoano,hata kama atacheza pira gimbi ila timu isonge mbele.

Muheshimu mpinzani kwa kufinya uwanja,kisha toka kwa Counter-attack uzuri una Mpanzu,Kibu na Mukwala ambao wanaweza kukimbia.

Hapa watanielewa wachache ila wenye uelewa wa mpira

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad