Web

𝐎𝐅𝐅𝐈𝐂𝐈𝐀𝐋: Kifungo cha Paul Pogba Kimeisha na Maisha Yanaendelea Japo Kwa Ugumu

𝐎𝐅𝐅𝐈𝐂𝐈𝐀𝐋: Kifungo cha Paul Pogba Kimeisha na Maisha Yanaendelea Japo Kwa Ugumu


🗣️Paul Pogba: “Pesa hubadilisha watu. Inaweza kuvunja familia. Inaweza kuunda vita. Wakati fulani nilikuwa peke yangu na nilihisi kama sitaki kuwa na pesa tena wala sitaki kucheza tena.

Nilitaka kuwa na watu wa kawaida, kwa hivyo marafiki na familia yangu wananipenda kwa ajili yangu, sio kwa umaarufu, sio kwa pesa.”

Paul Pogba Brothers wakiwa na magenge mengine kweli walienda kumuibia, kwa bahati mbaya wezi hao Paul Pogba aliweza kumtambua kaka yake kati yao licha ya yeye kuvaa barakoa (mask) 🎭.

Kwa nini ndugu waligeuka dhidi yake? Sababu ni hii; walihisi Paul hakuwa akiwapa pesa za kutosha licha ya kuwa mmoja wa wanasoka tajiri zaidi duniani, hivyo wakaanza kufanya kila kitu ili kumuangusha Paul Pogba, hata wakatoa siri ya jinsi Paul Pogba alivyoenda Afrika kufanya Voodoo 💔

Baadhi ya wanafamilia ni adui yako mkubwa, kuwa mwangalifu. Mtu anatakiwa kuwa makini sana siku hizi

𝐎𝐅𝐅𝐈𝐂𝐈𝐀𝐋: Kifungo cha Paul Pogba sasa ni kimeisha na anapatikana kucheza soka kuanzia leo ✨

Pogba, bado yuko sokoni kama mchezaji huru na yuko wazi kwa ukurasa mpya baada ya mazoezi ya mara kwa mara huko Miami…


Unahisi ni klabu gani inapaswa kwenda kumchukua Paul?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad