Miguel Gamondi, kocha wa soka mwenye umri wa miaka 58, ameamua kuachana na klabu ya Al Nasr SC ya Libya kwa sababu ya klabu hiyo kushindwa kulipa mishahara na ada zake. Gamondi alijiunga na klabu hiyo mnamo Februari, lakini sasa anatazamiwa kuwa kocha huru baada ya kutolipwa.
habari zinasema kuwa rais wa Al Nasr SC ameondoka klabu hiyo kufuatia mabishano yaliyotokea ndani ya klabu. Hali hii imeongeza misukosuko katika timu hiyo ya Libya.