Mameneja Habari na Mawasiliano wa vilabu vya Simba Sc na Yanga Sc, Ahmed Ally na Ally Kamwe wote wameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimaadili.
Wawili hao wameripoti asubuhi ya leo, Machi 3, 2025 kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume, Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza kusomewa makosa yao na hukumu.
Haya yanajiri zikiwa zimesalia siku tano tu kabla ya wawili hao kukumbwa na joto la Derby ya Kariakoo, pale wenyeji, Yanga Sc watakapochuana na Simba Sc katika dimba la Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi, Machi 8, 2025.