Kuna ufanano mkubwa sana kisifa za mchezo baina ya Aziz Ki na Jean Charles Ahoua...
Ahoua na Aziz Ki ni Profile zinazokupatia jawabu la kufanana kimahitaji kiwanjani ..
• Wote si mahiri sana kukokota mpira...wala kazi chafu bila ya mpira...
• Ila wote ni “masters” inapokuja suala la wapi wasimame au wawepo kupokea,kutunza au kutoa mipira kiwanjani kwa muda na wakati sahih ili kuathiri michezo kwa faida ya timu zao zinapomiliki mpira ama kujilinda....
• Aziz Ki kutumia mguu wa kushoto inaweza kutoa wazo la acheze winga wa Kulia ...lakini si eneo ambalo litamtambulisha vyema ubora wake...i.e uhuru wa kuzurura na kuyaona mashimo eneo la juu, kupokea mipira na kisha kupenyeza mipira ya mwisho ama kumalizia mashambulizi mwenyewe....
Ni jawabu la kufanana pia kwa Ahoua, ukimtumia kushoto kama winga... walau yeye ile kasi yake ndio humpa faida kufanya vema eneo hilo...lakini hakupi tija % huko wide... kama anayokupatia ukimtumia Shimoni nyuma ya mshambuliaji wa kusimama pale juu...
Ufafanuzi wa mdogo wangu @augustomalusu